26.6 C
New York

Kaka afunga mjadala, ataja bingwa Kombe la Dunia 2026

Published:

RIO, Brazil

KIUNGO wa zamani wa AC Milan, Kaka, ameipa timu yake ya Taifa ya Brazil nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu.

Fainali hizo zitaanza kutimua vumbi Juni 11 na kumalizika Julai 19, 2026, zikifanyika katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada.

Kwa mujibu wa Kaka, mbali ya Brazil kutwaa taji, nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, ndiye atakayeibuka Mchezaji Bora wa mashindano hayo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Kwa upande mwingine, amemtabiria Carlo Ancelotti anayeinoa Brazil kubeba tuzo ya Kocha Bora wa fainali hizo.

Wakati huo huo, Kaka amesema timu ya Taifa ya Marekani chini ya kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino, itafika nusu fainali.

Related articles

Recent articles