TORONTO, Canada
POLISI nchini Canada wanawashikikia watu wawili baada ya kuwakuta na mzigo wa jezi feki za fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazoanza Juni 11, 2026.
Ifahamike kuwa Canada ni moja ya wenyeji wa fainali za mwaka huu kwa kushirikiana na Marekani na Mexico.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa mzigo uliokamatwa wa jezi hizo ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Canada.
Polisi wametaja thamani ya jezi hizo ni Dola za Marekani milioni 2.53, sawa na idadi ya jezi zaidi ya 16,000.
Kwa mujibu wa polisi, jezi hizo zina chapa ya kampuni mbalimbali kubwa za Nike, Adidas na Puma, pia zikiwa na chapa ya FIFA.
Mji Mkuu wa Canada, Toronto, unatarajiwa kuhudumia mechi sita, ambapo utapokea mashabiki zaidi ya 300,000.


