21.2 C
New York

Huyu ndiye mchezaji ‘mzee’ zaidi Kombe la Dunia 2026

Published:

LONDON, Uingereza

ZIMABEKI siku tisa tu. Ni fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni 11, 2026 huko Marekani, Canada na Mexico, zikitarajiwa kufanyika kwa mwezi mmoja katika mataifa hayo.

Kwa mara ya kwanza, michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) itashirkisha timu 48 na kuwa wenyeji watatu kwa mpigo.

Kwa upande mwingine, mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Scotland, Craig Gordon, ndiye atakayekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika fainali hizo. Gordon ana miaka 43.

Kipa huyo aliyezaliwa Sikukuu ya Mwaka Mpya mwaka 1982, anaitumikia Hearts ya Ligi Kuu nchini Scotland. Alianza kuitumikia timu ya taifa Mei, 2024.

Hata hivyo, bado Gordon hatoweza kuvunja rekodi ya mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.

Rekodi hiyo bado inashikiliwa na mkongwe wa timu ya Taifa ya Misri, Essam El Hadary, ambaye alicheza Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi akiwa na umri wa miaka 45.

Related articles

Recent articles