24.5 C
New York

Gilberto Mora: Kinda wa kihistoria Kombe la Dunia 2026

Published:

LONDON, Uingereza

KUELEKEA fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazoanza Juni 11, 2026, macho yote ni kwa kiungo wa timu ya Taifa ya Mexico, Gilberto Mora.

Mora ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi msimu huu. Alizaliwa Oktoba, 2008, hivyo atashiriki michuano hiyo akiwa mchezaji pekee mwenye miaka 17.

Kwa sasa, nyota huyo anayekipiga Ligi Kuu ya Mexico akiwa na klabu ya Tijuana anawaniwa na vigogo wa soka la Ulaya, Real Madrid na Manchester United.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa Mora atakuwa mchezaji mwenye umri mdogo pekee kuwahi kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Itakumbukwa, Norman Whiteside wa Jamhuri ya Ireland ya Kaskazini alishiriki michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 17 na siku 41 mwaka 1982.

Related articles

Recent articles