LONDON, Uingereza
MASTAA zaidi ya 100 wa klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) watakuwa katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazoanza Juni 11, 2026.
Kama ilivyo kawaida, michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) itafanyika kwa mwezi mmoja na safari hii wenyeji ni Marekani, Canada na Mexico.
Je, ni klabu zipi za EPL zitakazowakilishwa na wachezaji wengi katika mashindano hayo yaliyoanza mwaka 1930? Endelea kusoma makala haya.
MANCHESTER CITY
Jumla ya nyota 15 kwenye fainali hizo. James Trafford (England), Abdukodir Khusanov (Uzbekistan), John Stones (England), Marc Guehi (England), Josko Gvardiol (Croatia), na Ruben Dias (Portugal)
Wengine ni Matheus Nunes (Ureno), Nico O’Reilly (England), Rodri (Hispania), Mateo Kovacic (Croatia), na Bernardo Silva (Ureno).
Pia, kuna Jeremy Doku (Ubelgiji), na Omar Marmoush (Misri), Rayan Cherki (France), na Erling Haaland (Norway).
ARSENAL
Nyota 14 wa Arsenal wameitwa na mataifa yao. David Raya (Hispania), William Saliba (Ufaransa), Gabriel Magalhaes (Brazil), Declan Rice (England), Martín Zubimendi (Hispania), na Martin Odegaard (Norway)
Wengine ni Gabriel Martinelli (Brazil), Leandro Trossard (Ubelgiji), Eberechi Eze (England), Bukayo Saka (England), Noni Madueke (England), Mikel Merino (Hispania), Kai Havertz (Ujerumani), na Viktor Gyokeres (Sweden).
ASTON VILLA
Jumla ya wachezaji 11 wa Villa watakuwa Kombe la Dunia. Emiliano Martínez (Argentina), Ezri Konsa (England), Victor Lindelöf (Sweden), na Lucas Digne (Ufaransa).
Wengine ni John McGinn (Scotland), Amadou Onana (Ubelgiji), Youri Tielemans (Ubelgiji), Emiliano Buendía (Argentina), Evann Guessand (Ivory Coast), Morgan Rogers (England), na Ollie Watkins (England)
MANCHESTER UNITED
Nyota 10 kwenye fainali za Kombe la Dunia. Senne Lammens (Ubelgiji), Altay Bayindir (Uturuki), Lisandro Martínez (Argentina), na Diogo Dalot (Ureno).
Wengine ni Diego Leon (Paraguay), Casemiro (Brazil), Kobbie Mainoo (England), Bruno Fernandes (Ureno), Matheus Cunha (Brazil), na Amad Diallo (Ivory Coast).
CRYSTAL PALACE
Klabu hiyo ina uwakilishi wa wachezaji 10. Dean Henderson (England), Walter Benítez (Argentina), Maxence Lacroix (Ufaransa), Daichi Kamada (Japan), na Ismaila Sarr (Senegal)
Wengine ni Jefferson Lerma (Colombia), Yéremy Pino (Hispania), Jorgen Strand Larsen (Norway), Jean-Philippe Mateta (Ufaransa), na Daniel Munoz (Colombia).
CHELSEA
Blues wana wachezaji tisa kwenye fainali hizo. Mike Penders (Ubelgiji), Mamadou Sarr (Senegal), Malo Gusto (Ufaransa), na Marc Cucurella (Hispania), Reece James (England).
Wakati huo huo, kuna Enzo Fernandez (Argentina), Alejandro Garnacho (Argentina), Pedro Neto (Ureno), na Nicolas Jackson (Senegal)
LIVERPOOL
Vigogo wa Merseyside watakuwa na nyota nane. Alisson (Brazil), Ibrahima Konate (Ufaransa), na Andy Robertson (Scotland).
Wengine ni Wataru Endo (Japan), Alexis Mac Allister (Argentina), Florian Wirtz (Ujerumani), Mohamed Salah (Misri), na Alexander Isak (Sweden).
NEWCASTLE UNITED
Nyota nane, ambao ni Malick Thiaw (Ujerumani), Dan Burn (England), Tino Livramento (England), na Bruno Guimaraes (Brazil).
Wachezaji wengine wa Newcastle watakaokwenda kwenye michuano hiyo ni Anthony Elanga (Sweden), Anthony Gordon (England), Yoane Wissa (DRC), na Nick Woltemade (Ujerumani).


