4.1 C
New York

Belarus yaachia wafungwa 123

Published:

MINSK, Belarus

SERIKALI ya Belarus imetangaza kuwaachia huru wafungwa 123, akiwamo wanasiasa wa upinzani, ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Marekani.

Marekani iliiwekea vikwazo vya kiuchumi Belarus, ikiushutumu utawala wake kukiuka haki za binadamu, hasa dhidi ya wanaharakati.

Ukraine imethibitisha kuwapokea wafungwa 114 walioingia nchini humo kwa hifadhi baada ya kuachiwa huko Belarus. Miongoni mwao ni aliyekuwa kiongozi wa maandamano, Maria Kolesnikova.

Wakati huo huo, Ukraine imeeleza kuwa wafungwa hao watapatiwa matibabu, kisha watachagua kwenda Poland au Lithuania.

Katika hatua nyingine, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema kati ya wafungwa hao, watano ni raia wa nchi yake waliokuwa wakifanya kazi katika mashirika ya misaada.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wafungwa wengine tisa wameshakimbilia Lithuania baada tu ya kutoka gerezani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img