9.8 C
New York

Bei ya tiketi Kombe la Dunia yazua gumzo

Published:

LONDON, Uingereza

MASHABIKI wa soka duniani kote wameendelea kulalamikia bei kubwa ya tiketi za kuingia uwanjani wakati wa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani.

Kwa baadhi ya nchi, bei ya tiketi kwa mechi moja ya hatua ya makundi ni kubwa kuliko kima cha chini cha mshahara wa Serikali.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilitangaza bei ya tiketi Alhamisi ya Desemba 11, mwaka huu, huku tiketi ya mechi za hatua ya makundi ikigharimu mara mbili ya kile cha fainali zilizopita.

Kwa mujibu wa FIFA, tiketi ya bei rahisi zaidi itapatikana kwa Dola 3119 (zaidi ya Sh mil. 7 za Tanzania), kiasi hicho kikiwa ni nje ya gharama za usafiri, makazi na malazi.

Mmoja ya mashabiki wa soka nchini Ghana ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa wengi wao watashindwa kwenda kwenye fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Wakati huo huo, FIFA wao wamemtangaza kuwa tayari kuna maombi milioni tano ya tiketi kutoka kwa mashabiki wa nchi zaidi ya 200 duniani kote.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img