9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi K

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi K na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Katika Kundi hili, zipo Ureno, Uzbekistan, Colombia na timu moja itakayofuzu kupitia ‘playoff’ kati ya DRC, New Caledonia na Jamaica.

Ureno, hata bila Cristiano Ronaldo imeonesha kuwa inaweza kufanya jambo, kama ilivyofunga mabao nane katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Armenia.

Hata hivyo, Japan ni tishio kwa Ureno katika Kundi hili, ikizingatiwa kuwa ndiyo timu iliyoruhusu mabao machache zaidi kwa upande wa Asia wakati wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia.

Colombia nao si wa kubeza. Walifika fainali msimu uliopita wa michuano mikubwa zaidi Kusini mwa Amerika, Copa America.

Ugumu wa Kundi hili unatarajiwa kuongezeka maa dufu endapo wawakilishi wa Afrika, DRC, nao watafuzu kupitia ‘playoff’.

Kwa upande wao, Uzbekistan waliofuzu wakiwa nafasi ya nne kwa upande wa Bara la Asia hawapewi nafasi ya kufanya maajabu kwenye fainali hizo za mwakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img