9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi D

Published:

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi D na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Ni Kundi lenye wenyeji Marekani, Paraguay, Australia na timu itakayofuzu kupitia ‘playoff’ kati ya Uturuki, Romania, Slovakia na Kosovo.

Mwezi uliopita, Marekani ilionesha ilivyoimarika chini ya kocha Mauricio Pochettino baada ya kuifunga Paraguay, na kisha kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Uruguay.

Marekani watacheza mechi yao ya kwanza kwa kuivaa Paraguay, ambayo hii ni mara yao ya sita kushiriki fainali za Kombe la Dunia.

Paraguay, ambao wamewahi kufika robo fainali mara moja, walifuzu wakiwa wamefunga mabao 14 katika mechi 18.

Australia wao walifuzu wakiwa kwenye presha kubwa. Walihitaji ushindi katika mechi zao mbili za mwisho na wakafanikiwa kuzifunga Japan na Saudi Arabia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img