9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi C

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi C na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Ni Kundi linalozikutanisha Brazil, Morocco, Haiti na Scotland. Kwa upande wao, Scotland wanarejea baada ya miaka 28 ya kuikosa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.

Mara ya mwisho kushiriki, walikuwa kundi moja na Brazil na Morocco na walipoteza mechi zote mbili dhidi ya miamba hiyo ya soka kutoka Amerika ya Kusini na Afrika.

Haiti wao hii ni mara yao ya pili kwani waliwahi kushiriki mwaka 1974, ambapo waliishia makundi wakiwa wamepoteza mechi zote tatu.

Brazil chini ya kocha wa zamani wa AC Milan na Real Madrid, Carlo Ancelotti, walifuzu, licha ya kupoteza mechi tatu mfululizo.

Kwa upande wao, Morocco wanarejea wakiwa na matumaini makubwa ya kuendeleza kile walichokifanya mwaka 2022 nchini Qatar.

Waliweka rekodi ya kuwa taifa la kwanza barani Afrika kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Safari hii, ‘Simba wa Atlas’ walijihakikishia tiketi wakiwa wameshinda mechi zao zote za kufuzu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img