9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi B

Published:

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi B na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani. Ni Kundi linalozikutanisa Canada, Qatar, Uswis na timu moja itayofuzu kupitia ‘play-off’ kati ya Bosnia, Ireland ya Kaskazini, na Wales.

Canada anafuzu kwa mara ya pili (baada ya mwaka 2022), ingawa historia ya Kombe la Dunia haitambui ushindi wowote waliowahi kuupata katika michuano hiyo.

Uswis, baada ya kushindwa kufuzu mwaka 1998 na 2002, wamevuka hatua ya makundi mara zote nne walizoshiriki Kombe la Dunia hivi karibuni. Safari hii, wamefuzu bila kupoteza mchezo.

Qatar, kwa upande wao, wako chini ya kocha wa kimataifa wa Hispania aliyewahi kuinoa Real Madrid, Julen Lopetegui. Walifuzu kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Falme za Kiarabu (UAE).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img