LONDON, Uingereza
MEYA wa Jiji la London, Sadiq Khan, amemwita Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni mtu aliyetawaliwa na ubaguzi wa rangi, jinsia na dini.
Khan ameibuka kujibu kile alichokisema Trump wakati wa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
Akizungumza Jumanne ya wiki hii, Trump alisema London imepata meya wa hovyo anayeweza kulipeleka Jiji hilo katika matumizi ya sheria za Dini ya Uislam (Sharia).
Akijibu kupitia mahojiano yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Khan alisema inaonekana Trump anaumia mno kuona London ikiwa chini ya meya wa Dini ya Uislam.
“Nafikiri Rais Trump ameonesha wazi kuwa yeye ni muumini mzuri wa ubaguzi wa rangu, kijinsia na hata dini ya Uislam,” alisema.
Wakati huo huo, Khan alisema si kweli kwamba London itaanza kutumia ‘Sharia’, na badala yake itaendelea kutumia sheria za Uingereza.
Meya Uingereza aibuka kumjibu Trump
Published:


