3.2 C
New York

Utafiti: Vijana wengi hawana nguvu za kiume

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

UTAFITTI mpya nchini Uingereza umebaini kuwa asilimia zaidi ya 65 ya vijana wenye umri chini ya miaka 40 wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nguvu za kiume. Ni utafiti uliofanywa na Taasisi ya Chemist4U, ukieleza kuwa tatizo ni kubwa zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 25 hadi 34.

Aidha, utafiti huo unaibua mtazamo mpya, tofauti na ilivyozoeleka kuwa ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo la wazee pekee. Kwa upande wake, utafiti wa Chemist4U ulihusisha vijana wa kiume zaidi ya 2,000 na nusu ya wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 walikiri kupitia changamoto hiyo.

Aidha, wengi kati ya hao walikiri kupitia utafiti huo kuwa wamekuwa wakitumia dawa, ikiwamo Viagra, ili kupata ‘heshima’ wawapo faragha na wenza wao. Ili kujiridhisha zaidi, wataalamu wa Chemist4U walifanya utafiti juu ya Viagra na kubaini kuwa ni moja ya dawa zinazowavutia vijana pindi wanapohisi kuwa na changamoto hiyo.

Mtaalamu wa afya wa Chemist4U, Ian Budd, anasema: “Kupitia ‘google’, tumeona namna vijana wanavyouliza maswali mengi wakitaka kujua kuhusu Viagra.”

Lakini, kwa mujibu wake, zipo sababu nyingi za vijana wa kiume kujikuta kwenye shida ya ukosefu wa nguvu za kiume. Anatolea mfano msongo wa mawazo, ulevi wa pombe na kutokufanya mazoezi.

Kwa upande mwingine, msomi huyo anashauri pia, kwamba ni sahihi zaidi kwa mtu mwenye changamoto hiyo ya ukosefu wa nguvu za kiume kupata msaada kutoka kwa wataalamu.

“Hutakiwi kujifungia ndani kukabiliana na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume …Wakati mwingine, ukosefu wa nguvu za kiume inaweza kuwa dalili ya matatizo makubwa ya afya kama shinikizo la damu, kiwango kikubwa cha mafuta mwilini na hata changamoto ya afya ya akili,” anasema Budd.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img