1.6 C
New York

Infographic| Ukatili dhidi ya wanawake bado mwiba nchini

Published:

Ripoti mpya ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) ya mwaka 2021 kuhusu Haki za Binadamu inaonesha kuwa bado ni mwiba.

Kwani licha ya kuwapo kwa unafuu wa matukio ya ukatili ikilinganishwa na miaka ya nyuma lakini bado juhudi zaidi zinahitajika katika kukomesha hali hiyo nchini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kupitia takwimu za Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI),Camilius Wambura, inabainisha kuwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake yaliyorekodiwa na polisi mwaka 2020 yaliongezeka kwa karibu matukio 3,000 ikilinganishwa na mwaka wa 2019.

Mnamo Julai 2021, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI),Camilius Wambura, alibainisha kuwa jumla ya watu 15,131 walikumbwa na matukio ya ukatili wa kijinsia katika kipindi cha Januari hadi Juni 2021.

Hiyo ilikuwa ni pungufu ya watu 4,209 (21.8%) ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2020.

Mwenendo kwa miaka mitatu.

Mwenendo wa ukatili dhidi ya wanawake kwa miaka mitatu kuanzia 2019 hadi 2021 unaonesha kuwapo kwa panda shuka.

Katika mwaka 2019 kulikuwa matukio 23,685 huku kiwango hicho kikiongezeka mwaka 2020 na kufikia 26,544. Huku unafuu ukionekana mwaka 2021 ambapo kulikuwa na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake kuwa 11,138.

Kanda hatari

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi hilo limebainisha kuwa katika kipindi hicho cha mwaka 2021, kanda ambayo ina kumbukumbu zaidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia ni pamoja na Arusha(1,697), ikifuatiwa na Ilala(1,486), Tanga(1,347), Kinondoni (924), na Lindi (780).

Aidha, takwimu za polisi kwa mwaka 2021 zinaonyesha kuwa jumla ya wanawake waliofanyiwa ukatili ni 11,138 ikiwa ni pungufu ya matukio 8,670.

Aidha, licha ya ongezeko hilo, idadi bado ni kubwa kama ilivyo hatari.

Hii ni sawa na wastani wa wanawake 1,490 wanaofanyiwa ukatili kila mwezi kote Tanzania.
Kwa maneno mengine ni kwamba wanawake 50 wanafanyiwa aina tofauti za ukatili wa kila siku.

Ni bayana kwamba juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa na kila aliyepo kwenye ngazi ya maamuzi ikiwamo wadau.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img