21 C
New York

Rais wa Finland ziarani nchini, Rais Samia ampokea

Published:

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb, amewasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kisha kukagua  gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Stubb yupo nchini kwa ziara ya kitaifa inayoanza leo Mei 14 hadi 16, 2025, kwa mwaliko rasmi wa Rais Samia.

Tanzania na Finland zimekuwa na uhusiano wa takribani miaka 60, zikiendelea kushirikiana katika sekta za elimu, misitu, mageuzi ya mifumo ya kodi, usawa wa kijinsia, pamoja na maeneo mapya ya ushirikiano kama mabadiliko ya tabianchi, ulinzi, uchumi wa buluu, akili unde na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img