21.8 C
New York

Utekelezwaji duni wa maagizo ya Kamati za Kudumu za Bunge

Published:

Na, Anoth Paul, Gazetini

KUMEKUWA na kusuasua kwa namna utekelezwaji wa maagizo ya Kamati za Bunge unavyosuasua kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Uwajibikaji – Usimamizi wa Taasisi za Umma 2020/2021., Kwa muujibu wa ripoti hiyo kunaongezeko la asilimia 23 kwa miaka miwili la maagizo ambayo hayatekelezwi pia kuna kushuka kwa utekelezwaji wa maagizo kwa asilimia 6.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanya kazi ya kuisimamia serikali kwa kuunda kamati zake za kudumu na hapa ndipo kamati hizi hufanya kazi ya kuandaa ripoti zenye mapendekezo yenye mlengo wa kuisimamia Serikali na Tasisi zake yanayotakiwa kutekelezwa na Watumishi/Watendaji katika Taasisi hizo, kamati hizi pia hufanya kazi pamoja na Taasisi ya Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) na Usalama wa Taifa ili kuhakikisha maagizo yanatekelezeka kama anavyoeleza Hamisi Kigwangala ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali.

Picha| Jengo la Bunge la Tanzania

Hata hivyo Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inayoangazia uwajibikaji  kwenye kipengele cha utekelezwaji wa maagizo ya kamati za bunge mwaka 2019/2020 imeonesha maagizo asilimia 37 ndio yaliyotekelezwa ikiwa maagizo yasiyotekelezwa yakiwa ni asilimia 43 wakati yanayoendelea kutekelezwa yakiwa asilimia 20 na yaliyopitwa na wakati hayakuwepo hali hii ni tofauti na ile ya mwaka 2018/2019 ambapo Maagizo yaliyotekelezwa yalikuwa asilimia 43 wakati yasiyotekelezwa yakiwa asilimia 20 na yale yanayoendelea kutekelezwa yalikuwa 34 ikiwa yaliyopitwa na wakati ni asilimia tatu. Kwa muujibu wa ripoti hiyo kunaongezeko la asilimia 23 kwa miaka miwili la maagizo ambayo hayatekelezwi pia kuna kushuka kwa utekelezwaji wa maagizo kwa asilimia 6. Ripoti inasema tatizo hili linasababishwa na ukosefu wa nidhamu ya kiutendaji kwa watumishi.

Mbali na ripoti hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Japhet Hasunga mara baada ya kikao cha Bunge kutathmini mwenendo wa utekelezwaji maagizo ya  Kamati zake akaeleza namna Kamati za Bunge zinavyofanya kazi katika kuhakikisha wanatimiza jukumu lao la kuisimamia serikali lakini pia katika maelezo yake amethibitisha kuwepo kwa utekelezwaji duni wa maagizo yanayotolewa na kamati hizo.

Kwa upande mwingine Hamisi Kigwangala ambaye yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni na pia ni Mbunge wa Jimbo la Zenga vijijini  hapa anatueleza namna utekelezwaji duni ulivyonamathara kwenye utawala bora na anagusia namna machakato mzima wa  maelekezo/maagizo yanayotolewa na kamati hiyo unavyokuwa, pia Kigwangala amesema “Bunge hutoa hukumu pia kwa Taasisi  zisizozingatia maagizo ya Kamati ili kuhakikisha utekelezwaji”.

Hata hivyo Simon Songe ambaye ni mbunge wa Jimbo la Busega hakusita kudokeza ushauri kwa watekelezaji wa maagizo wa Kamati za Bunge na bunge lenyewe na amesema kuwa kutotekelezwa kwa maagizo hayo kunaondoa imani ya wananchi kwa wawakilishi wao yaani viongozi ambao wanafanya kazi kwa niaba ya wananchi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img