8.5 C
New York

Serikali yatenga Bilioni 8 kusaidia watoto wanaotoka familia maskini

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Serikali imeanzisha Mfuko maalumu utakaowasaidia wanafuzni wanaotoka katika mazingira magumu ili waweze kumudu masomo yao nakupunguza utegemezi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Hayo yamebainishwa Jumanne Juni 14, 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 bungeni jijini Dodoma.

Amesema miongoni mwa sababu zinazosababisha kukatisha masomo kwa wanafunzi ni umaskini
wa kipato kwenye familia, mimba za utotoni, mwamko duni wa elimu kwa baadhi ya jamii na utoro na wale wasioendelea kufuatana kwa mujibu wa sheria (Ufaulu).

“Ili kukabiliana na utoro (drop out) wa wanafunzi wanaotoka familia maskini, bado tuna watoto
wanaoshindwa kumudu mahitaji ya lazima licha ya kuwepo kwa programu ya elimu bila malipo na hivyo wanasaidiwa na wabunge, madiwani na wengine kuchangiwa na wasamaria wema.

“Napendekeza kuanzisha dirisha maalum (Special Fund) kupitia TASAF itakayosaidia watoto wanaotokea familia maskini. Kwa msingi huo napendekeza kuanza na Sh bilion 8 kwa ajili ya watoto masikini watakaopatikana kwenye database ya TASAF na taarifa za wabunge na madiwani,” amesema Dk. Nchemba.

Kwa mujibu wa Dk. Nchemba, serikali imeendelea kugharamia programu ya elimumsingi bila ada
ambapo hadi Aprili 2022, jumla ya Sh bilioni 244.5 zilitolewa.

“Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameguswa sana na watoto kukatisha masomo kwa ajili ya sababu mbalimbali,” amesema Dk. Nchemba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img