4.5 C
New York

Nahodha: Ronaldo ni mzigo tu kwa sasa

Published:

RIYADH, Saudi Arabia

NAHODHA wa zamani wa Al Nassr, Hussein Abdulghani, amesema kwa sasa Cristiano Ronaldo si mchezaji anayeweza kuisaidia timu hiyo ndani ya uwanja.

Abdulghani amesema Al Nassr wamekuwa wakimchezesha ‘CR7’ ili afikishe mabao 1,000, hivyo kujikuta akiiumiza timu kutokana na kukosa kwake msaada kikosini.

Kwa mujibu wa mkongwe huyo aliyetwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia akiwa na Al-Nassr [2013 – 2015], timu hiyo imekuwa ikicheza hovyo kwa kuwa inalazimisha kumtumia Mreno huyo, licha ya kutokuwa na umuhimu wowote uwanjani.

Ronaldo ameshafunga mabao 987 katika maisha yake ya soka na hivi karibuni alikosa penalti katika kichapo cha mabao 3-1 walichokipata kutoka kwa Al-Ahli.

“Ronaldo ni mchezaji mkubwa lakini kwa sasa hawezi kuwa na mchango wowote,” amesema Abdulghani akihojiwa na kituo cha televisheni cha MBC1.

“Al-Nassr wanamuombea Ronaldo afikishe mabao 1,000 na hicho ndicho kinachoiumiza timu. Hakuna anayesema hilo akihofia mashabiki wa Ronaldo lakini ni tatizo kubwa kwa Al-Nassr.”

Related articles

Recent articles