16.8 C
New York

Emery akataa kazi United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, ameonesha kutokuvutiwa na mpango wa kujiunga na benchi la ufundi la Manchester United.

Presha ya kutimuliwa imeongezeka kwa kasi kwa kocha Michael Carrick, hasa baada ya Man United kufungwa mabao mabao 3-0 na Bournemouth.

Mbali na Emery, makocha wengine wanaoendelea kuhusishwa na mikoba ya Carrick pale Old Trafford ni Eddie Howe na Julian Nagelsmann.

Hata hivyo, akihudhuria sherehe za Ballon d’Or jijini London jana Oktoba 26, 2026, Mhispania huyo aliweka wazi kuwa hatokubali ofa yoyote kutoka Man United.

Kwa sasa, Emery aliyewahi kuzinoa Arsenal, Sevilla na Villarreal, ana mkataba na Villa utakaofikia ukomo mwaka 2029.

Related articles

Recent articles