LILLE, Ufaransa
MKONGWE wa soka, Simon Zenke, amezishangaa Arsenal na Manchester United kwa kushindwa kuharakisha usajili wa straika wa Super Eagles, Victor Osimhen.
Zenke amedai kuwa mshambuliaji huyo hakustahili kwenda Galatasaray endapo klabu hizo za Ligi Kuu ya England [EPL] zingekaza buti.
Osimhen alijiunga na klabu hiyo ya Uturuki akitokea Napoli baada ya Chelsea, Arsenal na Man United kushindwa kuinasa saini yake.
“Nilishangaa sana kuona klabu kubwa za Ulaya kama Arsenal na Manchester United, ambazo zilihitaji straika wakati huo, zilishindwa kumsajili,” amesema.
Tangu alipojiunga na Galatasaray, Osimhen amekuwa moto wa kuotea mbali, ambapo amefunga mabao 68 na kutoa asisti 19 katika mechi zaidi ya 80.


