14.7 C
New York

Guti hajakubali Kane kupewa Ballon d’Or

Published:

MADRID, Hispania

KIUNGO wa Real Madrid, Guti, ameibua mjadala baada ya kusema Harry Kane hakustahili kuwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.

Guti alienda mbali zaidi na kushangazwa na kitendo cha hafla ya tuzo hiyo kupelekwa London kwa mara ya kwanza baada ya miaka 70.

Hivyo, kwa mujibu wa Mhispania huyo, Kane kutwaa Ballon d’Or ulikuwa ni mpango ulioandaliwa mapema.

“Sherehe za Ballon d’Or zilipelekwa London … na mtu kutoka London akashinda. Ni jambo la pekee kiasi gani? alihoji Guti.

Kane kutwaa tuzo hiyo kumewashangaza wengi kwani Kylian Mbappe ndiye aliyekuwa akiongoza kwa wingi wa kura wiki chache kabla ya hafla kuanza.

Related articles

Recent articles