RIO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa Santos ya Brazil, Neymar Jr, huenda akakumbana na rungu la kufungiwa mechi sita.
Kwa mujibu wa ripoti, Neymar mwenye umri wa miaka 34 ameponzwa na kitendo chake cha kufunika mkono wakati akizungumza.
Neymar alilimwa kadi nyekundu kwa kosa hilo baada ya kukwaruzana na kiungo wa Bahia, Rodrigo Nestor, katika mchezo ambao Santos ilisinda bao 1-0 wikiendi iliyopita.
Baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya Brazil, Bahia walimshutumu Neymar wakisema huenda alitoa kauli za kibaguzi dhidi ya mchezaji wao.
Kwa upande wake, Neymar alijitetea akimtuhumu kiungo huyo kwa kuonesha mchezo usio wa kiungwana.


