14.7 C
New York

Pedro wa Chelsea kuikosa Liverpool

Published:

MERSEYSIDE. Uingereza

KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amethibitisha kuwa mshambuliaji wake raia wa Brazil, Joao Pedro, atakosekana katika mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya Liverpool.

Pedro hakucheza wakati Blues walipotandikwa mabao 2-0 na Tottenham katika mechi ya Ligi ya wikiendi iliyopita.

Sasa, Alonso amethibitisha kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.

“Joao amepata majeraha ya nyama za paja, atakosekana kwa wiki kadhaa,” amesema Alonso kuwaambia waandishi wa habari jijini London.

Wakati huo huo, mbali na kuikosa Liverpool, pia Alonso amekiri kuwa ni mapema mno kuthibitisha kuwa Pedro ataiwahi Manchester United.

Related articles

Recent articles