BERLIN, Ujerumani
UTAFITI uliofanywa na Taasi ya R+V ya mjini Berlin umebaini kuwa idadi ya wananchi wa Ujerumani wanaolalamikia ugumu wa maisha imeongezeka na kufikia asilimia 59.
Kwa mujibu wa utafiti huo, ni ongezezeko la asilimia 7, ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2025. Je, kwanini kupanda kwa gharama za maisha?
Akizungumzia hilo, mchambuzi wa siasa mjini Marburg, Isabelle Borucki, ambaye alihusika kama mshauri katika utafiti, amesema: “Bei ya bidhaa muhimu, zikiwamo nishati, makazi na vyakula, imepanda mno.”
Wakati huo huo, asilimia 52 ya waliohojiwa wanaona nchi yao ikiingia kwenye changamoto hiyo kutokana na kuzidiwa na wingi wa wahamiaji.
Kwa upande mwingine, asilimia 20 ya waliohojiwa katika utafiti walieleza wazi wasiwasi wao wa kupoteza ajira kipindi hiki. Ni idadi ndogo, ikilinganishwa na tafiti zilizopita.


