22.2 C
New York

Ripoti: Vifaa vya kujifunzia changamoto shuleni

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

SEKTA ya elimu imekuwa na tija kubwa katika maeneo ya mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla. Katika taifa lololote, mfumo bora wa elimu ndiyo uhai na uimara wa sekta zingine.

Sasa, kwa mujibu wa Ripoti ya Taasisi ya Uwajibika wa Umma [WAJIBU] ya Mwaka 2024-25, vifaa vya kufundishia, vikiwamo vitabu, bado ni changamoto kubwa katika shule nyingi hapa nchini.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kwa Mwaka 2024-25, kulikuwa na pengo la Shilingi bilioni 72.05 kwenye uwekezaji wa vitabu na mahitaji mengine ya elimu.

Wakati huo huo, Ripoti ya WAJIBU imeeleza pia kwamba uhaba wa waalimu ni changamoto nyingine inayoendelea ‘kuitafuna’ sekta ya elimu nchini.

Aidha, Ripoti pia imegusia changamoto za mrundikano wa wanafunzi darasani, pamoja na kukosekana kwa mfumo jumuhishi kwa wenye mahitaji maalumu.

Related articles

Recent articles