13.7 C
New York

Tofauti ya umri wa kuuziwa pombe duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

“HAIUZWI kwa mtu mwenye umri chini ya miaka 18.” Ni kaulimbiu maarufu katika matangazo ya kampuni za pombe. Kwamba bidhaa hiyo hairuhusiwi kisheria kuuzwa kwa mtu mwenye umri chini ya huo na imekuwa hivyo katika nchi nyingi.

Kwa mataifa mengi duniani, kama ilivyo Tanzania, Albania, Algeria, Andorra na Angola, umri huo umekuwa ukitumika kudhibiti wateja wa bia, lengo likiwa ni kuwakinga watoto wadogo.

Kwa sasa, ni nchi 13 pekee zinazotambua miaka 16, huku Burkina Faso ikiwa ndiyo pekee iliyoshusha umri hadi miaka 13.

Kwa mujibu Mfumo wa Taarifa za Pombe na Afya wa Umoja wa Mataifa, ukiacha Burkina Faso, nchi nyingine inayoruhusu mtu mwenye umri mdogo kununua bia ni Ivory Coast [14].

Mataifa mengine yanayotambua umri wa miaka 16 ni Austria, Ubelgiji, Denmark, Luxembourg, Dominica, Ujerumani, Grenada, Guyana, Luxembourg, Micronesia, Saint Lucia, San Marino, Sao Tome and Principe, na Uswis.

Hata hivyo, Malta ndiyo nchi pekee ya Ulaya, ambayo kwa sasa bado inatambua kuwa mteja wa pombe anaweza kuwa na umri wa miaka 17 tu.

Wakati huo huo, Eritrea inaendelea kuwa nchi yenye umri mkubwa kwa mtu kuruhusiwa kununua bia, ambapo ni miaka 25. Nchini Marekani, umri ni miaka 21.

Hali ni tofauti katika nchi za Afghanistan, Iran, Kuwait, Libya, Mauritania, na Sudan, ambako huko uuzaji wa pombe umepigwa marufuku moja kwa moja. Kwa Saudi Arabia, ni baadhi ya maeneo tu yanayoruhusiwa uuzaji.

Related articles

Recent articles