12.9 C
New York

Rapa Uingereza ana kesi ya ubakaji

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MWANAMUZIKI wa Hip hop, Yung Filly, atapandishwa kizimbani Juni, 2027, nchini Australia kujibu mashitaka ya ubakaji yanayomkabili.

Filly [31], alifunguliwa mashitaka hayo Julai, 2026, akitajwa kuhusika katika matukio matatu tofauti ya ubakaji.

Mmoja ya mashabiki wake ndiye aliyefungua moja ya kesi, akisema alibakwa na staa huyo akiwa na umri wa miaka 20.

Kwa mujibu wa bibiye huyo ambaye bado jina lake linahifadhiwa, alifanyiwa unyama huo mwaka 2024 katika moja ya vyumba vya hoteli mjini Perth, Magharibi mwa Australia.

Jina halisi la Filly ni Andres Felipe Valencia Barrientos na alizaliwa mjini Cali, Colombia. Akiwa na umri wa miaka miwili, alihamia London akiwa na mama na dada yake.

Related articles

Recent articles