11.9 C
New York

United, Liverpoo hazibanduki kwa Mitchell

Published:

LONDON, Uingereza

BEKI wa kushoto wa Crystal Palace, Tyrick Mitchell, bado anawindwa na klabu kongwe za Ligi Kuu ya England, Manchester United na Liverpool.

Mtandao wa TEAMtalk umeripoti kuwa Man United na Liverpool zinasubiri usajili wa dirisha dogo la Januari, 2027, ili kujaribu kuinasa saini ya nyota huyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amecheza mechi mbili akiwa na timu ya Taifa ya England lakini ana michezo zaidi ya 200 ya Ligi katika kikosi cha Palace.

Palace inaweza kushawishika kumuuza Januari kwani mchezaji huyo atakuwa mchezaji huru kiangazi, 2027, hivyo Man United au Liver inaweza kumnasa bure ifikapo kipindi hicho.

Liverpool wanaamini huyo ndiye mlinzi sahihi wa kuziba pengo la Milos Kerkez ambaye kiwango chake kimekuwa kikipanda na kushuka.

Related articles

Recent articles