LONDON, Uingereza
NI suala la muda tu. Arsenal wako kwenye hatua za mwisho za kumpa mkataba mpya kiungo wake raia wa England, Declan Rice.
Hatua hiyo inakuja baada ya kocha Mikel Arteta kusaini mkataba mpya utakaombakiza klabuni hapo.
Kwa upande wake, Rice anatarajiwa kupewa mkataba utakaomalizika mwaka 2028, na utakuwa na kipengele cha kuongeza mwingine wa mwaka mmoja.
Katika mkataba huo wa miaka mitano, kiungo huyo wa zamani wa West Ham United atajikunjia kiasi cha Pauni 280,000 kwa wiki.
Rice ni miongoni mwa wachezaji tegemeo kwa Arsenal na hata timu yake ya Taifa ya England, ambapo msimu uliopita [2025-26] alicheza mechi 69.


