15.5 C
New York

De Bruyne akanusha kuondoka Napoli

Published:

NAPOLI, Italia

KIUNGO wa Napoli, Kevin De Bruyne, amekanusha taarifa zilizodai kuwa alitaka kuondoka klabuni hapo wakati wa usajili wa kiangazi uliofungwa wiki chache zilizopita.

Wakati huo, ziliibuka ripoti zilizodai kuwa Mbelgiji huyo hafurahii maisha ndani ya klabu hiyo, hivyo anataka kuondoka.

Taarifa hizo zilienda mbali zaidi na kudai kuwa nyota huyo wa zamani wa Manchester City hakuwa na maelewano mazuri na kocha Antonio Conte.

Akijibu taarifa hizo, De Bruyne ameeleza kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo. “Hapana, sijawahi kuzungumza na yeyote [kuhusu kuondoka Napoli],” amesema De Bruyne.

De Bruyne alijiunga na Napoli ya Serie A mwaka jana akiwa mchezaji huru aliyemaliza mkataba wake na Man City.

Related articles

Recent articles