15.5 C
New York

Mbappe amzuia Olise kutua Madrid

Published:

MADRID, Hispania

STRAIKA wa Real Madrid, Kylian Mbappe, amesema winga Michael Olise kuondoka Bayern Munich kutakuwa ni kuivunjia heshima klabu hiyo.

Mbappe ameibuka na ushauri huo wakati huu Mfaransa mwenzake huyo akiendelea kuhusishwa na mpango wa kujiunga na Real Madrid.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Bild, Mbappe amesema: “Olise na Real Madrid? Nimesikia lakini utakuwa ni ushauri wa kuikosea heshima Bayern kumwambia aondoke …”

Wakati huo huo, Mbappe amedai kuwa Bayern, kama ilivyo Madrid, ni klabu kubwa, hivyo Olise anaweza kupata mafanikio makubwa akiwa hapo.

“Ndiyo, kila klabu duniani ingependa kuwa na Michael Olise. Ni mchezaji mzuri,” amesema Mbappe anayeshirikiana na Olise kwenye safu ya ushambuliaji ya Ufaransa.

Mkataba wa Olise na Bayern utakwisha mwaka 2029 lakini Madrid wanajaribu kuona kama wanaweza kuuvunja na kuipata saini ya mchezaji huyo.

Related articles

Recent articles