8.5 C
New York

Infographic| Idadi ya watu Afrika Mashariki kufikia mwaka 2050

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Rasmi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumanne ya Machi 25, 2022 waliidhinisha na kuikaribisha rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye uanachama mpya wa jumuiya hiyo inayokuwa na wanachama saba sasa.

Hii ni kufuatia mapendekezo ya kikao cha baraza la mawaziri cha Machi 25, kwamba Kongo imekidhi vigezo vya kujiunga na jumuiya hiyo kongwe barani Afrika baada ya mchakato wa muda mrefu.

Pia viongozi hao wamejiridhisha na faida za moja kwa moja za ushirikiano na taifa hilo kubwa kieneo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa pia na viongozi wengine wa jumuiya hiyo katika makao yake makuu yaliyopo Arusha Kaskazini mwa Tanzania.

Mwenyekiti wa wakuu hao wa nchi ambaye ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata, wakati akifungua mkutano huo alibainisha kuwa mkutano umebebwa na ajenda kuu ya wakuu ya kuikaribisha nchi Kongo DRC kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.

Marais wote kwa kauli ya pamoja wamesema baada ya kukamilika kwa hatua zilizosalia Kongo itakuwa rasmi mwanachama wa jumuiya hiyo.

“Waheshimiwa maraisi ninapenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana kwa kunikaribisha katika mkutano huu maalumu ambapo kwa mara ya kwanza ninazungumza kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kama mwanachama mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Rais Tshisekedi.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo iliyo na idadi ya watu wanaofikia milioni 90 na inayopakana na nchi tano za jumuiya hiyo, iliomba kujiunga na taasisi hiyo ya Februari mwaka 2021.

Kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo, nchi nyingine inaweza kujiunga iwapo itaungwa mkono na nchi wanachama na nchi hiyo inayoomba itakuwa imetimiza masharti ya uongozi bora, Demokrasia, Utawala wa Sheria, inayosheshimu haki za binadamu na kwamba iwe jirani na mojawapo ya nchi wanachama.

Idadi ya watu Afrika Mashariki kufikia mwaka 2050

Aidha, wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanaitazama Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa kufikia mwaka 2050 itakuwa na jumla ya watu milioni 583.

Aidha, Upande wa Kongo itakuwa na jumla ya watu milioni 195, ikifuatiwa na Tanzania watu milioni 129, Uganda milioni 100, Kenya milioni 92, Burundi milioni 25, Rwanda milioni 22 na Sudan Kusini milioni 20.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img