30 C
New York

Usiyoyajua kuhusu rapa aliyehukumiwa jela miaka 20

Published:

TEXAS, Marekani

WIKI hii imekuwa mbaya kwa mashabiki wa rapa Michael Lawrence Tyler maarufu kama Mystikal baada ya staa huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kosa la ubakaji.

Machi, 2026, mahakama ilimkuta na hatia, kabla ya hukumu yake kusomwa siku chache zilizopita.

Aliyemshitaki ni mwanamke aliyedai kuwa alibakwa na mshikaji huyo alipomfungia nyumbani kwake mjini Louisiana.

Mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu ya usalama, alidai kuwa Mystikal alimpokonya simu na funguo za gari.

Pia, kwa mujibu wake, Mystikal alichukua simu yake na kujihamishia fedha, kabla ya kumruhusu kuondoka kwenye mjengo huo.

Kabla ya hukumu, staa huyo alisema ikiwa ni kweli alitenda makosa hayo, basi apewe hukumu kali.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa wiki kadhaa zilizopita alijaribu kumshawishi bibiye huyo afute kesi, jaribio ambalo hata hivyo lilishindika.

MTU WA MATUKIO

Mystikal si mgeni wa kuta za gereza. Mwaka 2004, alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani katika mashitaka ya udhalilishaji wa kingono.

Mwaka 2012, aliingia tena gerezani, safari hii akihukumiwa miezi mitatu kwa kosa jingine la aina hiyo; unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Miaka mitano baadaye, mshikaji alirudi gerezani kwa kosa la kuteka mwanamke na kumbaka. Alikaa jela miezi 18.

NGOMA ZAKE

Mystikal alikuwa na mafanikio makubwa mwaka 2000 baada ya kuachia wimbo wake, ‘Shake Ya Ass’, kisha albamu ya ‘Let’s Get Ready’.

Let’s Get Ready itabaki kwenye historia ya muziki wa Hip hop baada ya kushika namba moja kwenye chati za Albamu kali nchini Marekani.

Rapa huyo hajaachia ngoma mpya kwa miaka 10 ya hivi karibuni na albamu yake ya mwisho ni Tarantula iliyoingia sokoni mwaka 2001.

Related articles

Recent articles