18.5 C
New York

Kama Senegal, timu hizi nazo zilipokonywa ubingwa

Published:

LONDON, Uingereza

HABARI kubwa iliyotikisa soka la Afrika ni timu ya taifa ya Senegal kuvuliwa ubingwa wa fainali za AFCON zilizomalizika miezi michache iliyopita.

Na badala yake, wapinzani wao, Morocco, wamepewa ‘ndoo’, licha ya kwamba walifungwa kwa penalti na Senegal katika mchezo wa fainali.

Senegal wameangukiwa na adhabu hiyo inayopingwa na wengi barani Afrika kwa kitendo cha wachezaji wake kugoma kuendelea na mchezo baada ya Morocco kupewa penalti ya dakika za majeruhi.

Hata hivyo, Senegal haiwi timu ya kwanza katika ulimwengu wa soka kuvuliwa ubingwa. Historia inatumbukusha timu tatu zilizowahi kufanyiwa hivyo.

Marseille (1992-93)

Marseille walibeba mataji makubwa mawili (Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa) msimu wa 1992-93. Wakavuliwa taji la Ligue 1 kwa kosa la kupanga matokeo.

Ni baada ya uchunguzi kubaini kuwa Rais wa Marseille, Bernard Tapie, aliwalipa fedha wachezaji wa Valenciennes ili wawarahishie kazi katika mechi iliyozikutanisha timu hizo.

Juventus (2004-05 & 2005-06)

Vigogo hao wa Serie A walipokonywa mataji yote mawili ya Ligi Kuu hiyo baada ya skendo ya kupanga matokeo.

Ikaelezwa kuwa meneja wa Juventus, Luciano Moggi, alikutwa na hatia katika uchunguzi uliobaini kuwa aliwalipa fedha waamuzi ili ‘waibebe’ timu yake. Juventus, mbali ya kupokonywa mataji, pia ilishuhushwa hadi Daraja la Kwanza (Serie B).

Genoa (2004-05)

Mechi yao ya mwisho ya Serie B (Daraja la Kwanza), ambayo Genoa walikuwa wanahitaji ushindi tu ili kutwaa ubingwa na kupanda hadi Serie A.

Dhidi ya Venezia, ilionekana Genoa wangepata ushindi kwa kuwa wapinzani wao hao walikuwa wameshashuka daraja na kutua Daraja la Pili.

Hata hivyo, licha ya Genoa kushinda na kutwaa ubingwa, iligundulika kuwa wakurugenzi wa klabu hiyo walimlipa fedha meneja wa Venezia, Giuseppe Pagliara, ili kazi iwe rahisi. Walilipa euro 250,000.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img