DHAKA, Bangladesh
VIWANDA maarufu vya nguo mjini Dhaka, Bangladesh, vimeshindwa kuendelea na uzalishaji baada ya wafanyakazi wake kuingia barabarani wakidai kulipwa mishahara midogo.
Taarifa zinaeleza kuwa viwanda takribani 150 vilifungwa Ijumaa ya wiki iliyopita katika miji ya Savar, Ashulia na Gazipur na havikufanya kazi wikiendi yote.
Biashara ya nguo ni chanzo kikubwa cha uchumi kwa wakazi wa mjini Bangladesh, ikitajwa kuzalisha takribani Dola bilioni 40 kila mwaka, huku ikichangia kwa asilimia 10 kwenye Pato la Taifa.
Katika maandamano yao, wafanyakazi wanashinikiza kima cha chini cha mshahara kifikie Pauni 182 kwa mwezi, lakini waajiri wanasema kiasi hicho ni kikubwa, ikilinganishwa na gharama za uzalishaji.
Asubuhi ya jana Novemba 15, 2026, maandamano hayo yalisababisha adha kubwa ya usafiri kwenye barabara kubwa za mjini Gazipur.


