Na mwandishi Wetu, Gazetini – LINDI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha mabasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi, akisisitiza kuwa mradi huo uwe chachu ya ajira, biashara na ongezeko la mapato kwa manufaa ya wananchi.
Akizungumza na wananchi leo Novemba 14, 2026, Ndejembi ameelekeza kujengwa kwa mzunguko wa barabara katika makutano muhimu ya Mtama, pamoja na kuandaliwa kwa mafunzo yatakayowawezesha vijana wa Lindi na Mtwara kunufaika na fursa zinazotokana na mradi wa gesi asilia ya LNG.
Aidha, amewataka viongozi kuchukua hatua dhidi ya watu wanaochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji ili wananchi waendelee na shughuli zao za kiuchumi kwa amani.
Makamu wa Rais yuko mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi, ambapo anakagua miradi ya maendeleo na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi.


