10.4 C
New York

TAKUKURU yatia mkono miradi ya bilioni 8.9/-

Published:

Na Editha William, Gazetini- KAGERA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Mkoa wa Kagera imefuatilia matumizi ya Shilingi bilioni 8.98 katika miradi 67 ya maendeleo kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, kwa kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Hajinas Onesphory.

Akizungumza leo Novemba 11, 2026, Onesphory amesema ufuatiliaji huo unalenga kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi na kuhakikisha uwajibikaji unaimarishwa.

Amesema taasisi hiyo pia imefanikiwa kurejesha Shilingi 277,801,365 kupitia kesi ilizoshinda mahakamani katika kipindi hicho cha miezi sita.

“Nitoe wito kwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuhakikisha inakamilika kwa ubora na thamani ya fedha za umma inalindwa.

Katika hatua nyingine, Onesphory amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuzuia ubadhilifu na kuhakikisha miradi inaleta manufaa yaliyokusudiwa kwa jamii.

Related articles

Recent articles