16.1 C
New York

Man United, Chelsea zawania beki Milan

Published:

MILAN, Italia

KLABU za Manchester United na Chelsea zinaiwania saini ya beki wa AC Milan ya Ligi Kuu nchini Italia [Serie A], Koni De Winter.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Milan msimu uliopita na sasa ameingia kwenye rada za vigogo barani Ulaya, ikiwamo pia Liverpool.

Katika hatua nyingine, maskauti wa klabu za Newcastle, Tottenham, Leeds United na Brentford nao wameripotiwa kumfuatilia.

Aidha, zipo ripoti zinazoeleza kuwa mchezaji huyo anatamani kubaki Milan, licha ya kusikia akihusishwa na klabu kubwa za Ligi Kuu nchini England.

De Winter amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, huku uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi kwenye ulinzi ukimfanya kuwa kivutio kwa maskauti wengi.

Related articles

Recent articles