21.8 C
New York

‘Upinzani si uadui, unaimarisha demokrasia’

Published:

LAGOS, Nigeria

NI kauli ya Mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia Chama cha Allied Peoples Movement [APM], Lawal Musa Daura, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Nigeria wa mwaka 2027.

Katika mkutano wake wa kampeni huko Abuja, Daura amesema upinzani ni kipimo sahihi cha namna serikali iliyoko madarakani inavyoweza kuhimili joto la kisiasa.

Hivyo, ameshauri serikali kuviona vyama vya upinzani kama msaada wa kujirekebisha na kona madhaifu, badala ya kuvitazama kwa jicho la uadui.

“Upinzani ni msaada kwa serikali, sio adui. Kama hakuna upinzani au mazingira mazuri kwa wapinzani, basi kuna tatizo,” amesema Daura.

“Demokrasia haiwezi kustawi katika mazingira ambayo wapinzani wa kisiasa wanaminywa na wananchi wananyimwa uhuru wa kuchagua vyama wanavyovitaka.”

Related articles

Recent articles