11.7 C
New York

Mchongo! Ukimpata Leijdekkers unalipwa bil. 5/-

Published:

AMSTERDAM, Uholanzi

MAMLAKA za Uholanzi zimetangaza ofa nono ya euro milioni 2 [zaidi ya Sh bil. 5 za Tanzania] kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya barani Ulaya, Jos Leijdekkers.

Leijdekkers [35], ambaye pia anafahamika kwa jina la Bolle Jos au Chubby Jos, anashitakiwa kwa kuendesha mtandao mkubwa wa dawa za kulevya aina ya cocaine ndani na nje ya Uholanzi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria wa Uholanzi, David van Weel, Leijdekkers ni mtu hatari kwa usalama wa Taifa, utawala wa demokrasia na hata sheria za kimataifa.

Nao waendesha mashitaka wa Uholanzi wameeleza kuwa kumkamata Leijdekkers ndiyo kipaumbele chao kwa sasa na atakayetoa taarifa zake atahakikishiwa usalama.

Januari, 2025, Leijdekkers alipigwa picha akiwa kanisani mjini Tihun, Sierra Leone, na polisi wa kimataifa walieleza kuwa amekuwa akitumia jina la Omar Sherrif kuficha uhalisia wake.

Katika picha za kanisani, Leijdekkers alionekana kuwa karibu na Rais wa sasa wa Siera Leone, Julius Maada Bio.

Ni baada ya picha hizo, waendesha mashitaka wa Uholanzi waliiomba Sierra Leone kumkamata na kuwakabidhi, ombi ambalo hata hivyo Serikali ya nchi hiyo ya Afrika ililigomea.

Related articles

Recent articles