TEHRAN, Iran
JESHI la Marekani limetekeleza mashambulizi mazito ya mabomu katika Kisiwa cha Qeshm nchini Iran na imethibitisha kufanya hivyo kupitia taarifa iliyotolewa na vigogo wake wa Serikali.
Kwa upande wake, Shirika la Utangazaji la Iran nalo limeripoti juu ya Marekani kufanya mashambulizi hayo jana Novemba 2, 2026.
Marekani imeeleza kuwa mashambulizi hayo ni majibu kwa jeshi la Kiislam la Iran [IRGC] lililoishambulia ndege yake.
Mashambulizi hayo yanakuja wakati Marekani ikikaribia kuingia kwenye Uchaguzi, huku Rais Donald Trump akikabiliwa na shinikizo la kuachana na vita dhidi ya Iran.
Aidha, hatua iliyochukuliwa na jeshi la Marekani inakinzana na ahadi aliyoitoa Rais Trump asubuhi ya jana Novemba 2, 2026, aliposema hawana mpango wa kuishambulia Iran kwa sasa.


