19.6 C
New York

Sakata la umeme lamuibua Makamu wa Rais Nigeria

Published:

LAGOS, Nigeria

MAKAMU wa Rais wa zamani wa Nigeria, Atiku Abubakar, amemjia juu Rais wa sasa wa nchi hiyo, Bola Tinubu, juu ya adha wanayopitia wananchi ya katikatika ya umeme.

Atiku aliyekuwa Makamu wa Rais wakati wa utawala wa Olusegun Obasanjo [1999 – 2007], kwa sasa ni mgombea wa urais katika Uchaguzi ujao kupitia Chama cha African Democratic Congress [ADC].

Kwa mujibu wa Atiku, wananchi wa Nigeria wamechoshwa na changamoto propagnda za utawala wa Rais Tinubu juu ya changamoto ya kukosekana kwa umeme wa uhakika.

Ameongeza kuwa badala ya kushughulikia tatizo, Serikali iliyoko madarakani imeendelea kujitetea, huku ikiongeza tozo kwenye huduma ya umeme.

“Visingizo vya Tinubu kuhusu umeme haviwezi kusaidia watu kupata umeme majumbani. Wanigeria wanataka umeme na si visingizio,” amesema Atiku.

Akisisitiza hilo, Atiku amesema uongozi wa Rais Tinubu unapaswa kuacha siasa, na badala yake kutafuta suluhisho la changamoto iliyopo.

Related articles

Recent articles