MICHIGAN, Marekani
LICHA ya upinzani mkali uliopo kati ya vyama hivyo, mwanasiasa wa Democrat, Haley Stevens, ameibuka na kumuunga mkono mgombea wa Republican katika Uchaguzi wa kiti cha Seneta wa Jimbo la Michigan.
Stevens alikuwa akiwania nafasi ya kuiwakilisha Democrats lakini Chama hicho kilimtupa na kumchagua mwenzake, Abdul El-Sayed, kugombea kiti cha Seneta.
Katika mazingira ambayo wengi hawakuyatarajia, Stevens aliibukia katika mkutano wa Republican jana Novemba Mosi, 2026, akiweka wazi kuwa yuko pamoja na mgombea wa Republican, Mike Rogers.
“Mimi si sehemu ya kampeni za Abdul,” alisema Stevens katika ujumbe wake kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter].
Baada ya kutangaza hatua yake hiyo, wafuasi wake kwenye mtandao huo walimuunga mkono na kusema wako naye bega kwa bega kumsapoti mpinzani wa Abdul wa Democrat.


