14.8 C
New York

De la Rose atamba AI kumfungulia milago upya

Published:

Na mwandishi wetu, gazetini

DE La Rose ambaye ni mwanamuziki na msanii wa maudhui ya mtandaoni, amesema hajaacha muziki kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria bali amejikita katika matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI) kuzalisha maudhui yaliyompa mashabiki wengi.

Akizungumzia mabadiliko hayo, De La Rose alisema yeye ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki na msanii wa sanaa za picha, hivyo anaamini ubunifu wake haupaswi kufungwa katika eneo moja pekee kwani AI inamwezesha kubadilisha hadithi, hisia na mawazo yanayochochea utengenezaji wa muziki wake kuwa picha na video ambazo mashabiki wanaweza kuziona na kuzipitia kwa namna tofauti.

“Nasisitiza kuwa teknolojia hii haichukui nafasi ya ubunifu wa binadamu, bali ni nyenzo inatusaidia kutekeleza mawazo yetu kama wasanii. Mfano ujumbe, hadithi au hisia zinazopatikana katika kazi zetu za kibunifu bado vinatokana na mimi mwenyewe, huku AI ikirahisisha uandaaji wa video ambayo kwa njia za kawaida yangehitaji gharama kubwa,” alisema De La Rose.

Aidha, msanii huyo anaona matumizi ya AI kama fursa muhimu kwa wasanii huru barani Afrika na kutoka katika jamii ambazo hazijapata uwakilishi mkubwa katika tasnia ya burudani ya kimataifa.

Related articles

Recent articles