12 C
New York

Halotel yaongeza kasi ya halofiber mara tatu

Published:

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam.

HALOTEL imeboresha huduma yake ya mtandao wa internet ya Halofiber majumbani kwa kuongeza kasi ya internet mara tatu zaidi ya kasi ya awali, huku gharama za huduma hiyo ikibaki vile vile.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Idara ya Fiber Majumbani, Fredy Ndabili, amesema Halofiber ilizinduliwa mwaka 2024 ikiwa na huduma katika mkoa mmoja, lakini hadi sasa imefika katika mikoa 22 nchini.

Amesema huduma hiyo sasa inapatikana katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Singida, Mbeya, Dodoma, Mtwara na Kigoma, huku kampuni ikiendelea na mpango wa kuwafikia watanzania wengi zaidi.

“Mapokeo ya huduma hii yamekuwa mazuri sana na tunafurahi kupokelewa vizuri. Tumeamua kuongeza kasi ya huduma ili kuwapa wateja huduma bora zaidi,” amesema Ndabili.

Amesema ongezeko hilo limefanya kasi ya Halofiber kuwa mara tatu ya kasi ambayo wateja walikuwa wakipata awali, huku gharama za huduma zikiendelea kuwa zilezile.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdallah Salum, amesema kampuni imefanya maboresho hayo kutokana na mahitaji na maoni ya wateja wake.

Amesema maboresho hayo yameongeza kasi ya intaneti zaidi ya mara tatu bila kuongeza gharama, akiwataka wateja waliopo kuendelea kutumia huduma hiyo na wengine kujiunga ili kunufaika na huduma ya intaneti majumbani.

Naye Balozi wa huduma hiyo, Ndutu J. Ndutu, amesema kuboreshwa kwa huduma hiyo kwa kuongeza kasi mara tatu huku bei ikibaki ileile kutawapa wateja thamani zaidi ya huduma wanayolipia.

Related articles

Recent articles