19.1 C
New York

Alaba atimkia Serie A

Published:

MILAN, Italia

BEKI wa zamani wa Bayern Munich na Real Madrid, David Alaba, amekubali kusaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Udinese ya Ligi Kuu ya Italia [Serie A].

Nyota huyo wa kimataifa wa Austria amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Madrid majira ya kiangazi, mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo wa Italia, Fabrizio Romano, Alaba ameshafikia makubaliano binafsi na Udinese.

Alaba, licha ya kuamua kuitumikia timu ya Taifa ya Australia, ana asili ya Nigeria, hivyo anakwenda kujiunga na kipa raia wa nchi hiyo ya Afrika, Maduka Okoye, katika kikosi cha Udinese.

Okoye, kwa upande wake, alisajiliwa na klabu hiyo Agosti, 2023, ambapo alisaini mkataba wa miaka minne.

Related articles

Recent articles