27.8 C
New York

Sababu 4 Alvarez kutua Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

STRAIKA wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, ameweka wazi kuwa anataka kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi.

Wakati Barcelona wakiwa wanapewa nafasi kubwa, zipo sababu 4 zinazowapa matumaini makubwa mashabiki wa Arsenal.

ATLETICO HAITAKI KUWAUZIA BARCA

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, uongozi wa Atletico uliweka mazingira magunu kwa Barcelona kumpata mashambuliaji huyo.

“Hakuna kiasi cha pesa ambacho Barcelona wanaweza kumsajili Julian Alvarez. Hatouzwa kwenda Barcelona. Labda kama watavunja mkataba wake kwa euro milioni 500, kinyume cha hapo hakuna biashara,” ilieleza taarifa ya Atletico.

Kuthibitisha kuwa Atletico haitaki kuwauzia wapinzani wake silaha, pia ilikataa ofa ya euro milioni 150 kutoka kwa Real Madrid.

DILI NJE YA HISPANIA

Si tu Barcelona na Real Madrid, bali Atletico haiko tayari kumuuza Alvarez kwa klabu yoyote ya Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga).

Kwamba kama staa huyo analazimisha kuondoka, basi atimkie Ligi Kuu ya England, Ufaransa, Ujerumani au Italia, na si kubaki Hispania.

Katika mazingira hayo, Arsenal inakuwa kwenye nafasi kubwa pia, licha ya kwamba PSG nayo imeripotiwa kuitaka saini yake.

OFA YA ARSENAL

Arsenal, mbali ya pesa, ofa yao kwa Atletico inahusisha pia mchezaji mmoja, huku Viktor Gyokeres na Ethan Nwaneri wakitajwa zaidi kwa wiki za hivi karibuni.

Wengine wanaohusishwa kufanywa ‘chambo’ katika dili hilo ni Gabriel Martinelli, Gabriel Jesus na Leandro Trossard.

Pia, zipo taarifa kuwa Arsenal wako tayari kutoa wachezaji wawili kwa mapigano endapo Atletico watapunguza dau katika meza ya mazungumzo.

ALVAREZ HAJAFUNGA MILANGO

Amesema tu anataka kuondoka Atletico lakini straika huyo hajataja klabu atakayojiunga nayo. Mlango uko wazi kwa Arsenal, kama ilivyo kwa klabu zingine.

Kwa kiwango chake, Alvarez anahitaji klabu ya daraja la juu, sifa ambayo Arsenal inayo kwa sasa, hasa baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya England na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2025-26.

Related articles

Recent articles