7.9 C
New York

Hizi ndizo ‘drone’ za bei rahisi inazotumia Iran kuzibomoa Marekani, Iran

Published:

TEHRAN, Iran

WAKATI Marekani ilipoanza kuishambulia Iran wiki chache zilizopita, Donald Trump alijitamba kuwa wataangamiza viwanda vyote vya silaha nchini humo.

Hata hivyo, Rais Trump alisahau kutaja ndege zisizo na rubani (drones) za Iran na sasa ndizo tishio kwao na kwa Israel.

Katika siku chache za vita, ambapo Marekani na Israel zinashirikiana, Iran imeshatumia ndege zisizo na rubani kushambulia maeneo zaidi ya 2,000.

Moja ya mashambulizi ya Iran yamefanywa nchini Kuwait, ambapo wanajeshi sita wa Marekani waliuawa.

Maeneo mengine ni Cyprus, Israel, Jordan, Iraq, Saudi Arabia, Bahrain, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Oman.

Iran inashambulia nchi hizo katika maeneo ambayo Marekani ina masilahi yake, zikiwamo kambi za kijeshi, hoteli, viwanja vya ndege, ofisi za balozi, na miundombinu ya nishati.

Je, unafahamu siri ya ndege zisizo na rubani zinazotumiwa na Iran?

Sasa, wataalamu wa masuala ya usalama wanasema ndege hizo zinafahamika kwa jina la Shahed.

Wanazitaja kuwa ni ‘drone’ zenye gharama ndogo na hata teknolojia inayotumika kutengeneza ni ya kawaida tu.

Mathalan, Shahed 136 ya masafa marefu, ambayo inatengenezwa Iran, inatajwa kugharimu kati ya Dola za Marekani 20,000 hadi Dola 50,000.

Tofauti na drone zingine, Shahed huwa haipewi maelekezo ikiwa angani, na badala yake kila kitu juu ya wapi inakwenda hufanyika ikiwa haijaanza safari.

Kwa makadirio, ni drone inayoweza kuruka hadi umbali wa kilometa 2,500, sawa na kutoka Tehran (Iran) hadi Athens (Ugiriki).

Licha ya kwamba haina kasi kama zingine, Shahed inasifika kwa uwezo wake wa kukwepa kusomwa kwenye rada za wapinzani iwapo angani.

Shahed, kwa wafuatiliaji wa vita zinazoendelea duniani, Urusi imekuwa ikizitumia drone hizo za Iran kuishambulia Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img