3.2 C
New York

Anayeshutumiwa kusuka mauaji ya Traore akamatwa

Published:

OUAGADOUGOU, Burkina Faso

RAIS wa zamani wa Burkina Faso, Paul-Henri Sandaogo Damiba, amekamatwa na vyombo vya dola vya Togo, na kisha kurejeshwa nchini kwake, ambako anakabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Sandaogo Damiba aliingia madarakani mwaka 2022 kwa mapinduzi ya kijeshi lakini alidumu miezi nane pekee, kabla ya kuondoshwa kwa mtindo huo huo na Ibrahim Traore.

Mapema mwezi huu, Waziri wa Ulinzi wa Burkina Faso, Mahamadou Sana, alitumia televisheni ya taifa kutangaza kuwa kulikuwa na jaribio la kuipindua Serikali na kumuua kiongozi huyo.

Sasa, utawala wa sasa wa Kapteni Traore unamshutumu Sandaogo Damiba kwa madai kuwa alikuwa sehemu ya waliohusika kusuka mpango wa kumuua Traore.

Kapteni Traore.

Kwa mujibu wa taarifa, Togo walikubali kumkamata Sandaogo Damiba alipoingia nchini kwao na kumrudisha Burkina Faso baada ya makubaliano kadhaa.

Miongoni mwa makubaliano yaliyoingiwa kati ya Togo na Burkina Faso ni kwamba kiongozi huyo atatendewa haki katika mashitaka yanayomkabili na hakutakuwa na adhabu ya kifo hata kama atakutwa na hatia.

Mbali ya kusuka mpango wa kumuua Traore, pia mwanasiasa huyo anashutumiwa kwa makosa ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img