2.9 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Uzbekistan (2)

Published:

LONDON, Uingereza
KWA viwango vya sasa vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Uzbekistan inashika nafasi ya 50.
Uzbekistan, maarufu kwa jina la ‘White Wolves’, haijawahi kutwaa taji lolote kubwa katika ulimwengu wa soka.
Kikosi hicho kinanolewa na beki wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italia, Fabio Cannavaro, ambaye amekuwa kwenye benchi la ufundi tangu Oktoba, mwaka huu.
Licha ya kwamba haina rekodi za kutisha, Uzbekistan ina kikosi chenye wachezaji kadhaa wanaocheza Ligi za Ulaya, wakiwamo Abdukodir Khusanov (Manchester City), Eldor Shomurodov (Istanbul Basaksehir) na Igor Sergeev (Pakhtakor).
Katika mechi za kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia hapo mwakani, Shomurodov ndiye aliyekuwa shujaa wao akifunga mabao matano.
Uzbekistan wamefuzu kwa mara ya kwanza baada ya majaribio saba tangu walipopata uhuru mwaka 1998. Walikaribia kufuzu mwaka 2006 na 2014 lakini hawakufanikiwa.
Kocha wa sasa, Cannavaro, ameikuta timu ikiwa imeshakata tiketi chini ya mtangulizi wake, Timur Kapadze, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo. Mkongwe huyo atakuwa kocha msadizi wakati wa fainali zijazo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img